Msanii Mad Ice anataraji kuzindua single yake mpya
inayokwenda kwa jina la wasiwasi siku ya Jumapili ya Tarehe 23 katika Ukumbi wa
Club Bilicanas katika usiku wa Bongo
Stars usiku
Usiku huo utasindikizwa na mtu mzima Fid Q
anaewaikilisha jiji la Mwanza kiburudani kinyumbani na kuwakilisha Taifa katika
Muziki Kiujumla.
Mad Ice ataachia single yake hiyo baada ya kukaa kmya
kwa muda mrefu katika Game la muziki kwa hapa nyumbani japo alikuwa kaiendelea
kufanya muziki akiwa nje ya Nchi
“Nina mashabiki kila idara, hilo sijalisahau na kamwe siwezi
kuwasahau kama wengi wasemavyo. Sasa mchongo uko hivi... Jumapili hii ya tarehe
23, tukune pale CLUB BILICANAS katika uzinduzi wa single yangu mpya
"Wasiwasi". Nitasindikizwa na mzee mzima FID Q, usikose show kali na
ya ukweli”







0 comments:
Post a Comment