Ummy Wenceslaus, alimaarufu kama Dokii, ndie anaeililia
nafasi ya kuimba mbele ya Rais Barrack Obama pindi kiongozi huyo wa Marekani
atakapo tua katika jiji la dare s salaam mwezi ujao.
Dokii anatamani kuimba nyimbo zake mbili za 'No One Like
Obama' na 'Obama Welcome to Tanzania' zinazotamba kwenye vituo mbalimbali vya
televisheni nchini kwa sasa.
Nyimbo hizo amezitunga maalum kwa kumpongeza na
kumkaribisha Tanzania Rais Baraka Obama mwenye asili ya Kenya.
"Nimekuwa nikitunga nyimbo kueleza sifa za Obama
tangu anaingia madarakani. Sasa naomba waandaji wa burudani wanipe fursa ya
kuimba mbele yake. Nitajisikia vizuri sana," alisema Dokii huku akiweka
wazi kwamba bado hajafanya mazungumzo na wahusika wa ziara ya Obama kuhusu ombi
lake.
"Kwa sasa niko kwenye mazoezi na 'madansa' wangu
tukiamini tutapatiwa nafasi hiyo."
Source Nipashe.







0 comments:
Post a Comment