Thursday, June 27, 2013

LAMAR AKUBALI KAZI YA AY NA FA AOMBA AIFANYE REMIX



Baada ya siku moja kupita toka kutambulishwa mkwaju mpya wa AY na FA huku wakiwa wamempa shavu mtu mzima J Martins kutoka pande za Nigeria, vocal plus Beat vikiwa vimetendewa haki na utundu wa Marco Chali Lamar akubali kazi iliyotendwa na wanamuziki hao na kuomba kuifanyia Remix.


Lamar kutoka Fishcrub amekili kuwa uwezo wa wasanii hao ni mkubwa na kazi waliotenda ni kubwa pia “Mziki wetu unakua kwa kasi sana big up to ay,mwana fa n jmartins 4 the sik tune!I need the vocals to do a rmx”

Cheza bila kukunja goti ni ngoma iliyopokelewa vizuri wa mashabiki ndani ya muda mfupi kwani imeweza kusambaa kwa kasi pindi tu ilipotangazwa siku ya jana.

0 comments:

Post a Comment