Mapenzi yatakuwa na wakati mzuri leo hii, furaha iliyopotea sasa inaweza kurejea na kukuweka kwenye matumaini na amani ya nafsi yako, Leo ni ijumaa nzuri kwa kufanya safari.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Siku ya leo unahitaji muda mwingi zaidi na tafakuri kabla ya kufanya maamuzi kwa mambo yaliyo mbele yako, ushauri si lazima kama unajiamini.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama unashindwa kuwa karibu na watu wanaokutegemea, basi waonyeshe njia na nini unafanya ili wajisaidie wenyewe, kwa kufanya hivyo utajikomboa na matatizo makubwa ambayo ungeweza kuyapata kutoka kwao.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Ni wakati wa kuwafungulia milango watu wapya kwa maana kuwa na marafiki wapya au ushirikiano mpya, mafanikio utayapata na mipango yako uliyonayo itaendelea kukuweka karibu na watu ambao usiowategemea kwamba wanaweza kuwa karibu na wewe.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Siku ya leo jaribu sana kujiweka mbali na migogoro nawa la usishiriki katika mamamuzi yatakayoonekana kuwa na mashaka kwa upande wako, leo ni siku ambayo unatakiwa uwe na furaha kwa sababu kila jambo lako litakwenda jwa wepesi kuliko ulivyotazamia.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Nguvu kubwa unayotumia katika kazi zako inaonekana kupungua, leo ni siku ya kufanya mabadiliko na kuwaongeza nguvu katika utekelezaji wa mabo yako siyo kukata tamaa wala kurudi nyuma.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Siku ya leo nafasi za mafanikio ziko mbele yako, jitihada zako zinaweza kuamua ni wapi unaweza kufanikisha ndoto zako, jipange sasa na tekeleza wajibu wako ipasavyo bila ya kukosa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Mawazo yako yanakupeleka mbali, lakini hata hivyo unahitaji kujituma zaidi na kuwashirikisha watu wengine katika maamuzi ambayo unataka kuyafanya, leo ni siku ambayo unatakiwa kuwa makini katika biashara unaweza ukapoteza fedha zako.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kauli zako zinaweza kuwa na maana isiyoeleweka mbele za wengine, kwa kuepuka matatizo kuwa makini katika maongezi yako.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Ijumaa ya leo wale ambao watakuzunguka watakuwa na mambo nya muhimu kuongea na wewe, lakini katika hayo si kila jambo linaweza kukufurahisha kuna mengine yatakuudhi lakini kuwa na subira na tumia busara katika majibu yako..
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Siku ya leo achana na wale ambao utaona wana nia mbaya, weka mkazo kwenye kazi zako na maamuzi yako yabaki kuwa kauli ya mwisho
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Pamoja na juhudi kubwa unayofanya, bado kazi zako zinakwenda polepole, kukata tamaa liwe jambo la mwisho kwa upande wako.
Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hasan.







0 comments:
Post a Comment