Dorice ambaye ni mwanafuzi wa mwaka wa pili
katika chuo cha Kumbumbumbu ya Mwalimu Nyerere ni mmoja ya wanafuzi 10 kutoka
nchini waliochaguliwa kwenda mjini Hamburg na Berlin kudumisha ushirikano na
kujifunza tamaduni za Kijerumani.
Mratibu wa Miss Tabata, Joseph Kapinga
alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na MitOst
Hamburg ya Ujerumani na Tanzania Youth Coalition.

“Tunashukuru sana hii ni nafasi pekee kwa
Dorice kujifunza mambo mengi kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Ilala
ambalo limepangwa kufanyika Agosti. Tuna imani ziara hii itapanua mawazo yake
na atakuwa tishio kwenye shindano hilo la urembo,” alisema Kapinga.
Dorice ambaye alishinda taji la Miss Tabata
Mei 31, aliondoka nchini Juni 6 na atarejea Julai 5.







0 comments:
Post a Comment