Tunapokuwa
kwenye mahusiano ya mapenzi na hata nyakati ambazo mahusiano yetu
yanapitia misuguano na tunalazimika kuachana yatupasa tuwe macho sana
katika “tunahusianaje” na “tunaachanaje”.
Nina
mifano hai ya baadhi ya watu ambao walifikiri mwisho wa ubaya
walioutenda wakiwa kwenye mahusiano fulani ungeishia kwenye mahusiano
yale tu na wakafikiri mara baada ya kuachana na mpenzi wa zamani na
kuanza na mahusiano na mpenzi mpya basi kila kitu kingekuwa shwari
kwasababu ya kale yamepita, kwa bahati mbaya yale mabaya
waliyoyapanda katika mahusiano yao ya awali yamekuja kuwarudia katika
mahusino mengine.
Walitesa,
sasa wanateswa, waliumiza, sasa wanaumizwa, walidhulumu, sasa
wanadhulumiwa, walidhihaki, sasa wanadhihakiwa, walionea, sasa
wanaonewa, na walitenda sasa wanatendwa. Kila unalotenda katika
mahusiano yako fahamu kwamba unapanda mbegu, na kama unapanda mbegu
basi fikiria pia na wakati wa kuivuna. Always kumbuka kuwa “what
goes around comes around”.
Imeandaliwa na Chris
Mauki







0 comments:
Post a Comment