KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo ukiwa katika matembezi yako kuna jambo la kukushangaza litakutokea, hiyo ni dalili kuwa mambo yako mengi yapo kizani, unashauriwa kuwa muwazi kwa kila jambo unalotaka kulifanya, usiri wowote unaweza kukusababishia hasara ambayo hukuitegemea.
Leo ukiwa katika matembezi yako kuna jambo la kukushangaza litakutokea, hiyo ni dalili kuwa mambo yako mengi yapo kizani, unashauriwa kuwa muwazi kwa kila jambo unalotaka kulifanya, usiri wowote unaweza kukusababishia hasara ambayo hukuitegemea.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Ikitokea Leo mtu yoyote akaja kwako kutaka ushauri, hiyo ni dalili ya kupendwa na watu hasa kama mtu huyo atakuja nyakati za asubuhi na kukukuta hujatoka nje, kuwa mwangalifu nyakati za jioni, Unashauriwa kutotoka kwa matembezi nyakati hizo.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo ndugu yako unayempenda ambaye anaishi mbali na wewe akikutembelea au ukikutana naye ghafla, hiyo ni dalili kuwa wewe si mtembeleaji wa wenzio, Unashauriwa kuwa mtembeleaji wa wenzio ili kuvuta bahati yako.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo Kuna watu watakujia kutaka kukupa msaada. Jitayarishe kuwapokea. ikitokea katika matembezi yako ukamuona Bundi, hiyo ni dalili ya kukimbiwa na mpenzi wako au rafiki yako unayemuamini kwa kila kitu.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo ukimtembelea mtu na ukamkuta anasoma gazeti au kitabu, hiyo ni dalili kwamba mambo yako yatakwama, hasa kama ulikuwa unamtgemea mtu mwingine kukufanyia hayo mambo yako.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo ukimkuta mtu anatembea akiwa ameshika mbuzi aliyefungwa kamba, hiyo ni dalili kuwa huko uendako si salama, unashauriwa kuwa mpole kwa kila jambo litakalokutokea, kwani ubishi kidogo tu utakusababishia kesi kubwa au kipigo.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo kuna dalili kwamba uhusiano wako wa karibu uliokuwa nao kati yako na mpenzi wako utavunjika. Sababu yake itakuwa maneno ya kuambiwa. Ili kuepusha hilo jaribu sana kufanya uchunguzi wa kila jambo la kimapenzi utakaloambiwa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Hivi sasa unafikiria sana kuhusu taabu mashaka au Matatizo yaliyopo kwa upande wa Mkeo au mumeo au mchumba wako au watu unaoshirikiana nao. Kuna habari utaletewa ya ugonjwa au Mgonjwa, makelele, Ugomvi na taabu ya wazee wako au wakubwa fulani katika Serikali au Kazi.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Muda huu mawazo yako ni namna utakavyowasilisha hotuba katika mkutano au ofisini una hamu ya kujua ni jinsi gani ya kutoa msaada kwa hao waliokuomba uwasaidie. Hapo ulipo una mipango ya kupata pesa na unafikiria jinsi mipango hiyo itakavyokamilika. Mambo yako yatakuwa kama unavyotaka
PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
LEO utasumbuliwa na maradhi ya mgongo na magoti yako yatakusumbua kidogo. Kubwa zaidi inaonekana una mgogoro mzito na Wazee wako, mkeo, mwanawake wako, mumeo au mwanaume wako.tafuta wazee mpate suluhu au utangamia.
NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Leo Una wasiwasi juu ya mali yako kuchukuliwa, au kazi yako kuharibika au kitu chako kupotea.Elewa kwamba adui yako utamshinda na kama una kesi utashinda, ugonjwa unaokusumbua utapona na barua au ujumbe unaotegemea utapata.
MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Iku ya leo Marafiki zako unaowatafuta au kuwahitaji utakutana nao, watakuletea faraja na mipango mizuri ya kimaisha,kamatana nao na wasikilize wale wanayotaka na utafanikiwa,
Imeandaliwa
na Mtabiri Maalim Hassan






0 comments:
Post a Comment