Wednesday, June 26, 2013

JOH MAKINI KUTAMBULISHA NIKUMBATIE




Mkali wa Muziki wa Hip Hop anaewakilisha kundi la Weusi Kampuni kutoka pande za Arusha JoH Makini A.k.A mwamba wa Kasikazini siku ya Ijumaa atakuwepo katika Ukumbi wa Ambassadors Lounge akitambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la NIKUMBATIE.


Ingawa mwamba hajaweka wazi humo ndani ya nikumbatie kunani lakini dhahili ujumbe huo unakwenda kwa mtoto mzuri maana katika hali halisi si rahisi kwa mtoto wa kiume kuomba ukumbatiwe na mtoto wa kiume mwenzake ila tunahitaji kukumbatiwa na warembo wazuri  

NIKUMBATIEya Joh Makini ama  Mwamba wa Kaskazini amempa shavu Msanii na Producer Fundi Samweli

“Ijumaa hii nitakua Ambassadors lounge kuitambulisha ngoma yangu mpya ''NIKUMBATIE''Feat.fundi samweli kwa show kaali na muziki mzuri”

0 comments:

Post a Comment