MAPACHA - GEMINI
(MAY 23- JUN 23)
Siku ya Leo kuna dalili ya kupoteza kitu chako muhimu ambacho kimekusaidia kwa muda mrefu. Mali iliyoibiwa siku nyingi itapatikana. Ikitokea leo wakati wowote ukamwona Panya mahali kwa hiyo ni dalili ya kupata misukosuko.
Siku ya Leo kuna dalili ya kupoteza kitu chako muhimu ambacho kimekusaidia kwa muda mrefu. Mali iliyoibiwa siku nyingi itapatikana. Ikitokea leo wakati wowote ukamwona Panya mahali kwa hiyo ni dalili ya kupata misukosuko.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo hii kuna ishara ya kufanikiwa katika mambo yako ya kikazi, adui yako atakuogopa na kukupisha ufanye mambo yako bila ya wasiwasi.usiwe na wasiwasi mkabili na upambane nae.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo hii ukimuona mtu ana ndevu nyeupe, basi ujue hiyo ni ishara ya kuwa mambo yako sasa yatafunguka na kukunyookea, ile mikwamo ya hapa na pale itafunguka kwa urahisi.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo katika matembezi yako ukikutana na mwanamme amevaa mkufu wa shanga, hiyo ni dalili ya kupata kila kitu utakachokihitaji bila ya kutumia muda au nguvu nyingi.Unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa sadaka.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo Mchana ukikutana na Mwanamme akiwa amevaa Mkufu wa Fedha, hiyo ni dalili ya kutimia kwa ndoto yako ya kupata Mwanamke au Mwanamme mzuri na kutimia kwa Ndoa yako
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ukimwona mtoto Leo hii analia, basi hiyo ni ishara ya wewe kupata mtoto mzuri au utapata mpenzi mpya ambaye utakutana naye bila ya kutegemea. Sherehe utakayohudhuria itakutanisha na wangu wengi ambao hukutegemea.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Elewa kuwa ile posa yako imekataliwa na mpenzi unayemtaka hana haja na wewe. Unahitajika kuwa mkweli kwa kila hatua utakayoichukua.ili hao unaowataka wakuamini na upate ukitakacho.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo hii ukipewa habari kwamba kuna mtu anakusengenya, hiyo ni dalili kwamba utakosa yale yote uliyoyategemea na mtu yoyote hawezi kuwekea pingamizi.tegemea kukutana na mtu mkubwa Serikalini ambaye atakusaidia.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Kama Leo hii ukiumwa kichwa au ukikutana na mtu akakuambia anaumwa kichwa, hiyo ni ishara ya kupata habari nzuri. Leo Mkeo au mumeo au mwanao atakuudhi kwa mambo atakayofanya..
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo utatukuzwa kwa jambo dogo utakalolifanya lakini utapata matatizo katika malengo yako uliyoyapanga kwa wiki nzima.Kuna watu wanataka kukukwamisha jaribu kuwa msiri wa mambo yako.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Elewa kuwa hutafanikiwa katika mambo ya pesa utakayoyafanya leo.Ili kuepuka hayo jitahidi kumuomba mungu kwa sala. Leo Jicho likikucheza au ukikutana na mtu ambaye ameumia Jicho, basi hiyo ni dalili ya kuwa msaada unakuja.
NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Leo hii ukimuona Paka katulia mahali wakati si kawaida yake, basi ujue hiyo ni dalili ya kuwa hauko mbali na mahali ambapo mpenzi wako huwa anakutania na mpenzi wake mwingine.
Imeandaliwa n Mtabiri Maalim Hasan
0 comments:
Post a Comment