Mchezaji Uhuru Seleman aliekuwa akiichezea timu ya Azam Fc
kwa msimu uliuopita wa Ligi kuu Bara kwa sasa Amejiunga na Timu ya Coastal
Union ya jijini Tanga kwa mkopo akitokea Azam FC alipokuwa akisakata Kabumbu
kwa msimu uliokwisha wa Ligi.
Uhuru kabla ya kutangaza rasmi kujiunga na Kikosi Hicho cha
Coastal Union kwa ajiri ya Msimu ujao wa ligi alifanya utafiti ili kujuwa
anapaswa kwenda kucheza timu gani na kwanini anakwenda katika timu hiyo na
alifanya hivyo wazi kulinda na kukuza kipaji chake kama mchezaji,moja ya timu
ambazo alionesha kuhitaji kwenda ilikuwa ni Simba Sports Club,Coastal Union
pamoja na Azam.
Nakumbuka Uhuru aliandika “Leo Mei 24 nimetimiza miezi sita
tangu nilipotua Azam, naomba mnisaidie nienda wapi Coastal Union, Simba au
Azam.” Baada ya wadau kumpa ushauri wengi wao walimshauli kurudi Simba Sports
Club na haijawa hivyo niklitaka kujuwa sababu za yeye kutojiunga na Timu yake
ya Simba aliyokwisha ichezea msimu wa Nyuma
Na majibu yake yalikuwa hivi “ni kweli9 nilitaka ushauri
kutoka kwa mashabiki wangu ambao wao ndio wanaonipa moyo na hamasa ya kufanya
kazi nzuri zaidi na walinishauri na nilichukua maamuzi yao ila nimeamua
kujiunga na Coastal Union ya mjijini Tanga kwa kuwa natambua nikiwa Coastal
Union nitafanya makubwa kisoka kwa kuwa naamini nitakuwa na nafasi ya kuonesha
uwezo wangu”
0 comments:
Post a Comment