Baraza
la Wazee wa klabu ya Young Africans wamesema kuwa hawana wasiwasi juu
ya kuifunga timu ya Simba Soccer siku ya Tarehe 18 Mwezi huu kwani
wanadai kua timu yao ya Yanga ndio timu bora kwa Mwaka huu na ndio
timu yenye wachezaji wazuri na ni Kikosi kilichokamilika kabsaaa.
Akiongea
na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao makuu ya
klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali
(Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yangaa kitaibuka na
ushindi katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata
sheria zote 17 na kanuni za soka.
Akilimali
amesema Yanga ni timu bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna wachezaji wazuri wenye kiwango
cha hali ya juu ambao wamepikwa wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo
yao ndio yaliyotupatia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Aidha
aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba tutamfunga Simba SC siku ya mei
18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na uongozi bora chini ya
mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga ambao mpaka sasa
wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda wote huuu".
Naye
Mzee Hashim Mwika aliongeza "Mwaka jana walitufunga kwa sababu
hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja
kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa
kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema
mzee Mwika
0 comments:
Post a Comment