Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) imetoa taarifa kuwa kinywaji cha Soda
hakina sumu kama ambavyo taarifa zilivyozagaa hivi karibuni katika
mitandao ya jamii nchini zikionesha Athari ya kinywaji hicho kwa
mtumiaji kuwa kina sumu.
Mamlaka
inamashaka na taarifa iliyotolewa kwa sababu haidhani kama ilitolewa
kwa kuzingatia misingi ya kisayansi .
Mamlaka
inawatoa hofu watumiaji wa kinywaji Hicho kuwa Soda ni bidhaa ya
chakula ambayo inatumika duniani kote na inatengenezwa kuzingatia
viwango vya ubora na usalama kwa matumizi.
TFDA
Soda zote zilizosajiliwa zimepitia katika mchakato ambao unatoa
uhakika juu ya usalama wake kwa lengo la kulinda afya ya Binadamu .
0 comments:
Post a Comment