Msanii
wa RnB kutoka Tanzania Ben Paul ambae ni mzawa wa Dodoma amedai kuwa
amekosa raha kusikia msiba wa msaniii mwenzake Albert Mangwea ambae
alikuwa akiwakilisha Dodoma katika Game na kama mtu aliewapa
Inspiration kufanya muziki hivyo kutokana na msiba huo amearisha
kutoa Video yake mpya inayokwenda kwa jina la JIKUBALI ambayo
alipanga kuiachia Wiki hii.
Kwa
mujibu wa Ben Paul alipanga kuiachia Video hiyo wiki hii na ameamua
kupisha Shughuli za mazishi ya Msanii Huyo na zitakapo kwisha ndipo
ataachia Kichupa Hicho cha jikubali.
“Sidhani
kama ninayo raha ya kutoa video yangu mpya wiki hii, naomba radhi,
nitapisha shughuli za mazishi ya ndugu yangu “
Alimaliza
kwa kusema restInPeace Albert
0 comments:
Post a Comment