Tuesday, May 21, 2013

RIZIKI YA LINEX IMEREKODIWA SIKU ALIYOFARIKI BIBI KIDUDE



Wimbo mpya wa mwanamuziki Linex unaokwenda kwa jina la Riziki yangu aliempa shavu Mwanamuziki kutoka Kenya anaewakilisha kundi la Necessary Noise Wyre ulirekodiwa siku aliyofariki nguli wa muziki wa Taarabu Fatuma Baraka(Bikidude).

Kwa mujibu wa Linex amesema kuwa yeye alipata taarifa ya kifo cha Bikidude akiwa studio anarekodi wimbo huo wa Riziki yangu na alipokea taarifa hiyo kwa masikitiko.

Siku kadhaa baada ya kuitambulisha ngoma yake hiyo mpya ya Riziki yangu imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya habari.

Na haya ni maneno machache yanayopatikana katika ngoma hiyo
Riziki yangu inapatikana usiku mkubwa wa manane mpaka nitupe ndoano ziwani ndio nipate chochote,maisha yangu unayajua baby utanivumilia kwenye shida na raha Ahhhaahh”.

0 comments:

Post a Comment