Rais
wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi amekabidhiwa lesseni
ya Mchezaji wa Yanga Emmanuel Okwi na shirikisho la mpira wa
miguu
Afrika.
Jamal
Malinzi amesema hayo leo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter
baada ya kutoka katika kikao cha utambulisho kwa Rais wa CAF Issa
Hayatou na katibu mkuu el Amrani, Malinzi aliambatana na Rais mstaafu
wa shirikisho hilo Tanzania Leodeger Tenga .
Jamal
malinzi ameahidi kuwapa Klabu ya Yanga Lesseni hiyo ya Mchezaji wao
Emmanuel Okwi kipindi atakaporudi Tanzania.
“CAF
wamenipa leseni ya Emmanuel Okwi, nikirudi nchini nitawakabidhi
Yanga”
0 comments:
Post a Comment