Mwanamuziki
wa Hip Hop kutoka jiji la New York Marekani Rick Ross ameomba msamaha
kwa watu wake na wanaharakati mbalimbali kufuatia wimbo wake
U.O.E.N.O aliouachia mwezi wa pili mwaka huu kuwa na msitari
unaohamasisha vitendo vya ubakaji.
Msamaha
aliomba Rick ni baada ya wanaharakati mbali mbali siku ya jumanne
kwenda Reebok store iliyopo Manhattan na kutoa mwongozo kwa
watengenezaji wa bidhaa za michezo kumtoa Ross kama msanii maarufu wa
kuiwakilisha kampuni hiyo katika bidhaa zake.
Katika
wimbo huo Ross ame rap kwa kusema “weka kilevi kwenye shampeni
yake,hawezi hata kujuwa,namchukua mpaka nyumbani kwake na
kufaidi,bila hata yeye kujuwa.
“tumewataka
Reebok kuvunja biashara na Rick Ross”amesema Shawna Thompson
msemaji wa wanawake wa Ultra Violet,kikundi cha haki ya za wanawake
kilichofanya maandamano siku ya jumanne akitoa sababu ya kwanini
wameamua kufanya hivyo ni kutokana na wimbo huo kuhamasisha vilevi na
ubakaji kwa wanamke.
Baada
ya sakata hilo Ross Jumanne hii aliomba msamaha kupitia ukurasa wake
wa twitter aliposema kuwa “SIFANYI VITENDO VYA UBAKAJI.Naomba
msamaha kwa misitari iliyotafisiliwa na kuhusishwa na vitendo vya
ubakaji.
SOURCE:CNN







0 comments:
Post a Comment