Thursday, April 4, 2013

MWAKYEMBE ADAIWA KUKIUKA TARATIBU

Waziri wa uchukuzi na usafilishaji Dr.Harrison Mwakyembe amekiuka sheria kwa kukiuka masharti ya utoaji zabuni kwa kuipa kampuni inayomilikiwa na CCM zabuni ya ujenzi wa mradi wa maegesho ya magari makubwa na makontena.
Inasemekana kuwa ameipa zabuni kampuni inayoitwa Jitegemee Trading Company Limited inayomilikiwa na CCM na gharama za Mradi huo utagharimu Sh.billion 10.
mbali na kutoa zabuni hiyo Mwakyembe amedaiwa kupeleka mradi huo kujengwa kwenye eneo la shirika la Uchumi na Kilimo Tanzania SUKITA ambalo pia linamilikiwa na CCM lililopo Eneo la Tabata.
Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Singo Kigaila, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema mradi huo ni kitu kizuri, lakini cha msingi, ambacho kinapaswa kuhojiwa, unajengwa wapi, na nani na kiasi gani taratibu zimefuatwa.

Kigaila alisema Halmashauri ya Temeke awali, ilitaka kuingia ubia na Bandari kujenga mradi huo kwenye eneo la Kurasini, karibu na Bandari, lakini Mwakyembe ameliacha eneo hilo na kuupeleka kwenye eneo la Sukita.




0 comments:

Post a Comment