![]() |
| ZITTO KABWE |
Wabunge
wameendelea kuibana Serikali katika vikao vya kamati za bunge
vinavyojadili mapendekezo ya Bajeti ya Wizara mbalimbali.
kumekuwepo
na mvutano mkubwa kati ya wabunge juu ya mapendekezo hayo hali
inayoashiria kuwepo kwa mvutano mkubwa katika Bunge la Bajeti
linalotarajiwa kuanza tarehe 9 mwezi huu wa nne mjini Dodoma.
Misuguano
ambayo ilijitokeza jana ni baina ya Kamati ya Hesabu za Serikali
(PAC) ambayo ilimgomea Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa kupunguza
Bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG).
Wakati
hayo yakiendelea vile vile Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira
ilikataa kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) ya Sh42.7 bilioni kwa maelezo kwamba fedha hizo ni kidogo
sana.
Kwa
upande wa Mawasiliano Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Makame Mbarawa aliiwekea ngumu Kamati ya Miundombinu, ambayo
ilikuwa ikitaka kuongezwa muda wa matumizi mfumo wa analojia hadi
2015, badala ya mwaka huu.







0 comments:
Post a Comment