Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernad Membe leo
akizungumza na waandishi wa Habari ameitaka nchi ya Malawi kuacha
kutapatapa na kuheshimu Makubaliano walioyoyafikia kuliachia jopo la
usuluhishi la SADC kufanya kazi yake.
“Serikali
ya Malawi iache kutapatapa. Waheshimu Makubaliano yetu ya kuliachia
jopo la usuluhishi la SADC lifanye kazi yake”
Membe
aliendelea kueleza kuwa makubaliano kati ya Tanzania na Malawi suala
la kwenda au kutokwenda ICJ kutategemeana na hitimisho la Jopo la
usuluhishi na sio vinginevyo
Wakati
jopo la usuluhishi linaendelea na kazi yake,mpaka itakavyoamuliwa
vinginevyo, mpaka ulioko katikati ya Ziwa uheshimiwe na usiguswe







0 comments:
Post a Comment