Wednesday, April 17, 2013

MIAKA YA KICHINA IME EXPIRE

Lulu Michael Muigizaji wa kike alietingisha jiji la dar es salaam na viunga vyake kwa skendos mbalimbali zikiwemo kudanganya jamii juu ya umri wake,mahusiano yake na kushiriki katika kumbi za starehe akiwa na umri usiotambulika katika viwanja hivyo,leo ameibuka na kusema kuwa miaka yake ya kichina ime expire.

Kauli hiyo ya mwigizaji LuLU imekuja kufuatia kutambua kua ameshadanganya sana katika jamii juu ya umri wake halisi mpaka kupelekea utata juu ya umri wake katika kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia,lakini ameamua kuweka wazi juu ya umri wake halisi ili jamii itambue na kuona kuwa mwanzo alikuwa akidanganya jamii.

Mpita Njia najiuliza swali Miaka aliyoandika katika Keki iliyoandaliwa kwenye party yake leo ni miaka yake halisi?kama yake halisi anasababu ipi kuitaja huku akitambua mwanzo alikuwa akidanganya jamii?je ni kutaka kuweka sawa kweli au anasababu nyingine?Napita tuu Mpita Njia naendelea na safari yangu..........

0 comments:

Post a Comment