Friday, April 5, 2013

MGOGORO WA ZIWA NYASA SERIKALI KUTOA TAMKO LEO

Serikali ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania inatarajia kutoa tamko kuhusu Ziwa Nyasa kufuatia Serikali ya Malawi kujitoa kwenye Mazungumzo ya usuluhishi yaliyokuwa yakiendelea baina ya nchi ya Tanzania na Malawi.
Juzi Raisi wa Malawi Joyce Banda alisema kuwa hajalidhishwa na mchakato wa usuluhishi uliokuwa unaendelea kati ya Tanzania na Malawi na kusema kuwa suala hilo analipeleka katika Mahaka ya Kimataifa (ICJ)
waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernad Membe jana amesema kuwa Serikali itatoa tamko leo wenye Msimamo wa suala la Mgogoro huo kati ya Malawi na Tanzania.

0 comments:

Post a Comment