Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Marekani
itafuatilia kwa makini hatua za viongozi wateule wa Kenya katika kukidhi
matakwa ya mahakama ya uhalifu ya kimataifa -ICC- kutokana na tuhuma
zinazowakabili.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari msemaji wa wizara hiyo Hilary Renner amesema watashiriki ipasavyo katika
kulifuatilia suala hilo.
Kutokana na kauli hiyo Sudi Mnette amezungumza na
Geofrey Musila, mwanasheria wa kimataifa na mchambuzi wa siasa za Kenya,
aliyejikita hasa katika masuala ya ICC na kwanza anaelezea kwanini marekani
imeibuka na suala hili wakati huu.
Kuskiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika
za masikioni hapo chini.







0 comments:
Post a Comment