Mchana huu Mbunge wa jimbo la bumburi Mh January Makamba
amefunguka na kusema kuwa Rushwa haitajilishi tu yule anaepokea bali inauwa
wale wasio na hatia yoyote.
Makamba ameyasema hayo kufuatia kuanguka kwa jengo jana
asubuhi na kuwawa Raia wasio na hatia na kujeruhi wengine
“Dua zangu kwa wote ambao wamefukiwa na kifusi baada ya
kuporomoka kwa jengo jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Familia za ndugu zetu hawa zinapitia kipindi cha huzuni kubwa
sana”
Aliendelea kuzungumza huku akionesha ishara ya kukiukwa kwa
mambo mengi katika ujenzi wa jengo hilo uliokuwa ukiendelea siku ya jana asubuhi kabla
ya kuleta maafa ya kuanguka na kuuwa raia
“Kanuni za ujenzi za kiwango cha juu kabisa haziwezi kuizidi
nguvu ya ulafi na tamaa ya binadamu! Rushwa haimtajirishi yule tu anayeipokea
lakini pia inaua wale wasio na hatia”
Alimaliza kwa kusema hivi “Muuza maziwa anaongeza maji kwenye
maziwa, kila mtu anamuongopea mwenzake! Jamii inayoongopa inatengeneza utumishi
wa umma ulio sawa na jamii yenyewe”.







0 comments:
Post a Comment