4:42 AM
Wadau wa
elimu wamesema mengi. Laiti wangesikilizwa, hali ya elimu nchini isingefika
hapa ilipo. Kwa bahati mbaya sana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
haikutoa nafasi kwa mawazo ambayo hayatokani na wao wenyewe, au watu ama
taasisi wanazozichagua kuzisikiliza.
Usipoziba ufa, utajenga ukuta. Hatimaye Tanzania
tumeanza kujenga ukuta. Tungeweza kuziba nyufa mapema-kuliko sasa
tunapolazimika kujenga ukuta. Sio kutokana na matokeo mabaya tu; ufundishaji na
ujifunzaji umeshuka sana katika shule zetu na hali ya elimu nchini inazidi kuwa
mbaya; hasa kuanzia elimu ya awali na ya msingi.
Hebu sasa mdau sema angalau jambo moja muhimu ambalo
TUME YA MH. PINDA; au serikali kupitia wizara ya elimu wanapaswa kulizingatia.
Wana-HakiElimu tumeanzisha kampeni hii ya kukusanya jumbe fupi fupi za wadau
kwa picha; au kwa maandishi; ambazo tutazikusanya na kuzifikisha kwa wadau.
TUTUMIE PICHA YENYE UJUMBE AU MAANDISHI MAFUPI SASA.
0 comments:
Post a Comment