![]() |
| SAMWELI SITTA |
Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Samweli Sitta amepinga shutuma zilizotolewa na baadhi ya
wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kutoka Tanzania kuwa Wizara yake haina ushukirikiano dhidi ya wabunge hao
wawapo kazini.
Wajumbe hao walidai
kuwa Sita hana ushirikiano mzuri kwa
wabunge hao wanapokuwa katika shughuli za kikazi, wabunge hao walitoa malamiko
hayo Jumanne kabla ya kikao cha kamati ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa kukaa.
Akijibu malalamiko
hayo Naibu Waziri wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki Dr Abdullah J ADDULLAH alisema
malalamiko hayo hayana ukweli wala uhalisia kwani Waziri amekuwa wazi katika
utendaji wake,na amekuwa akifanya kazi kubwa ila tatizo lipo kwa wabunge
wenyewe.
Baada ya kikao kuisha
sitta alikusanya nyaraka zilizoonyesha jinsi alivyokuwa akiwapa taarifa za
vikao wabunge hao na walikuwa wakishindwa kuudhuria vikao hivyo kwa kutoa
udhuru.







0 comments:
Post a Comment