Mbunge wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji ametoa pole leo kufuatia
jengo lilianguka kuuwa na kujeruhi watu katika eneo la makutano ya barabara ya
Morogoro na Idra ghand jijini Dar es salaam.
Mbunge huyo ameonesha kuguswa na kuumizwa na tukio hilo
lililotokea leo majira ya asubuhi na kusababisha vifo kwa watu zaidi ya kumi
mpaka sasa na kujeruhi watu zaidi ya thelathini ambao wameokolewa wakiwa Hai na
kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Mhimbili kwa matibabu zaidi.
“KUANGUKA KWA GHOROFA HAPA DAR: Mungu awape nguvu majeruhi
wote, Mungu azilaze mahala pema roho za waliopoteza maisha na tunakuomba Mungu
ndugu zetu waendelee kuokolewa wakiwa hai! Pole nyingi kwa wafiwa, jamaa na
marafiki. Ni msiba wetu sote”Amesema Shy-Rose.
Kufuatia zoezi la uokoaji linaloendelea katika eneo la tukio
kwa mujibu wa ripoti zilizopo mpaka sasa zaidi ya watu kumi wameripotiwa
kufariki dunia na wengine zaidi ya thelathini wameokolewa wakiwa wazima ila ni
majeruhi waliokimbizwa hospitali.







0 comments:
Post a Comment