Source:Mwanchi Web
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Joseph Haule, a.k.a Profesa Jay, amesema hajashangaa kujikuta katika
orodha ya mwanzoni kabisa ya wanamuziki wa heshima waliotajwa kushiriki tamasha
lililoandaliwa na mwanamuziki nguli kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone.
Jay ambaye kwa mujibu wa
Chameleone mwenyewe, ataambatana na mwanamuziki mwingine aliyewahi kuwika na
miondoko ya Takeu, Lucas Mkenda, au Mr Nice, amesema heshima kama hizi haziji
hivi hivi ila zinatokana na kuhangaika kwake na muziki huu wa kizazi kipya na
kuhakikisha kwa kila njia unafika katika hatua nyingine.
Katika mahojiano yake maalumu
aliyofanya na Mwananchi, Jay amesema ukiachana na suala la muziki, yeye ni kama
kaka wa wanamuziki kwa sasa.
Jay ambaye kwa sasa anasikika
katika vituo vingi vya redio kupitia nyimbo zake nyingi ukiwamo ule
alioshirikishwa na Lady Jaydee wa Joto na Hasira, anatajwa kuwa mwanamuziki
aliyetia ushawishi wa hali ya juu kwa wasanii wachanga kuanza muziki hapa
nchini.
Onyesho hilo linatarajia pia
kukusanya na wanamuziki kutoka Kenya, litafanyika katika siku tatu mfululizo
ambapo siku ya kwanza, itakuwa ni tarehe 26 Aprili, katika viwanja vya mchezo
wa rugby vya Kyandondo jijini Kampala, kisha Colline Hotel siku itakayofuata
katika Mkoa wa Mukono na litafuatiwa Entebe tarehe 28 katika fukwe za Resort
Beach.






0 comments:
Post a Comment