Lakini pamoja na sababu alizozitoa
Malima kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Sulemani Kova amesema
polisi pamoja na bodi ya makandalasi na
bodi ya waandisi watashirikiana kwa ukalibu kuchunguza tukio hilo kwa kina
zaidi.
Kuanguka kwa jengo hilo jana si mara
ya kwanza katika historia ya tanzania hivi kalibuni kwani mwaka 2008 lilianguka
jengo lenye ghorofa kumi maeneo ya kisutu na kujeruhi watu,vilevile mwaka 2006
lilidondoka lingine maeneo ya chang’ombe na kujeruhi watu na bila kusahau juzi
juzi hapa kunajengo limedondoka kinondoni na kujeruhi watu na mali zao
Nikuache ukiendelea kutafakari na
kujiuliza kama tatizo ni vifaa vya ujenzi vipo chini ya kiwango maana havina
ubhora je mamlaka husika kama TBS ziko wapi na zinafanya kazi ipi?je hivyo
vifaa ni kwamba vinaingia kwa njia zipi mpaka vishindwe kuzibitiwa?je viongozi wetu kweli wanamapenzi ya kweli kwa
sisi wananchi wa hali ya chini kabsaa au wanafanya kazi kwa masirahi yao
binafsi?






0 comments:
Post a Comment