Polisi zanzibar wametoa taarifa kuwa
wamemkamata Omar Mussa Makame mwenye umri wa miaka 35 wakimtuhumu kuwa ndie
aliehusika na mauaji ya padri Evaristus Gabriel Mushi alie uwawa kwa kupiga
Risasi siku ya Jumapili 17 mwezi wa pili alipokuwa kaielekea kuongoza Misa.
Kamanda wa polisi Zanzibar Mussa Ali
Mussa amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekatwa jana katika maeneo ya Kariakoo
kufuatiwa uchunguzi mkali wa kipolisi uliofanyika na kumpata
Sakata hilo limefuatia baada yua
siku mbili toka kardinali Pengo kuwatuhumu polisi kwa uwezo mdogo na kushindwa
kabisa kumkamata mtuhumiwa alihusika na mauaji ya padri Mushi.







0 comments:
Post a Comment