Saturday, March 30, 2013

BUMBULI KUPATA HALMASHAURI YA WILAYA


Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga linaloongozwa na Mh January Makamba limepata Halmashauri ya Wilaya

Akizungumza juu ya suala hilo Mbunge wa Jimbo hilo Mh January Makamba amesema kuwa imemchukuwa miaka miwili kufanikisha suala hilo

“Hatimaye suala nililolipigania kwa miaka miwili limefanikiwa kwani Jimbo la Bumbuli sasa limepata Halmashauri ya Wilaya

Kwa mfumo wa utawala wa nchi yetu,maendeleo yanapangwa, kusimamiwa na kutekelezwa katika ngazi ya Halmashauri”.

Mbunge huyo aliendelea kuzungumza kuwa baada ya kujing'atua kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, sasa tutakuwa na rasilimali nyingi zaidi za maendeleo, tutakuwa na eneo dogo zaidi la usimamizi wa shughuli za maendeleo (tulipokuwa ndani ya Halmashauri ya Lushoto tulikuwa Kata 44.

Sasa tutakuwa Kata 16 tu), tutasogeza huduma za kiutawala na kijamii karibu zaidi na watu, na tutasukuma maendeleo kwa kasi zaidi. Kazi iliyo mbele yetu sasa ni kuisimamia vizuri hii Halmashauri ili malengo yetu yatimie. Kazi hiyo tutaifanya.

Uzinduzi wa Halmashauri hiyo mpaya itakuwa ni Tarehe 24 Februari 2013.


0 comments:

Post a Comment