Wednesday, March 20, 2013

MWAKYEMBE-INJINI MPYA ZITAPUNGUZA GHARAMA ZA TRENI

DR HARRISON MWAKYEMBE
Waziri wa Uchukuzi,  Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali inahitaji injini za kisasa ili kuboresha usafiri wa treni kwa mkoa wa Dar es Salaam na reli ya kati kwa ujumla ili kupunguza gharama za uendeshaji wa usafiri huo.

Dk. Mwakyembe  ameyasema  hayo  (jana) wakati akiongea na wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea mradi wa reli wa kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam .

“iwapo injini hizo zitapatikana  Serikali itapunguza gharama kubwa izitumiazo kuendesha usafiri huo kwa sasa  kwa kuwa injini zilizopo zinatumia mafuta mengi wakati za kisasa zinatumia mafuta machache na zinakwenda kwa kasi.
Waziri wa uchukuzi aliendelea kuelezea kuwa

“Gharama za injini hizi ni Dola za Kimarekani milioni 6 ambazo Serikali imeshindwa kuzipata  kutokana na uwezo mdogo wa kifedha iliyonayo .Hivyo basi juhudi za pamoja zinahitaji baina yetu sote  ili kuiboresha sekta hii ambayo ni mhimili wa ukuaji wa uchumi wa nchi” .

msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Midladjy Maez alidai  gharama za uendeshaji  mradi  ni kubwa, hivyo aliomba kuboreshwa  kwa njia za treni,pamoja na kumalizia ujenzi wa vituo vya stesheni za njiani.

 “Kwa wakati huu TRL haiwezi kumudu gharama za uendeshaji wa treni hii, kwa hiyo tunaiomba Serikali itoe ruzuku ili TRL iweze kupunguza hasara inayoipata kila mwezi.










0 comments:

Post a Comment