Timu
ya Azam FC leo wanajitupa kiwanjani tena kusaka alama ntingine tatu muhimu. Leo
Azam FC watakuwepo Mlandizi kupambana na Ruvu Shooting ya Pwani.
Mechi itapigwa kwenye uwanja wa Mabatini kama
kawaida na kikosi cha Azam FC kipo makini kwani Wachezaji wote wako timamu
ukiondoa mlinda mlango namba moja Mwadini Ali anaesumbuliwa na mafua
Vilevile
wachezaji kama Abdulhalim Humudi hata
kuwepo kikosini leo kwani yupo kwenye majaribio Jomo Cosmos na David Mwantika ambaye
anatumikia kadi nyekundu.
Lakini
Faraja kubwa katika kikosi cha leo ni kurejea kikosini kwa Brian Umony ambaye
ameyashinda majeruhi yaliyokuwa yanamsumbua.






0 comments:
Post a Comment