Na Gerald Kitalima
Msanii alietamba kwa muda
mrefu na ngoma yake ya Mwana AliKiba kesho anaratajia kuachia wimbo
wake mpya unaokwenda kwa jina la
Chekecha,kupitia ukurasa wake wa
Intragram baada ya kuonyesha picha inayoonyesha ujio wake mpya
mashabiki wa Ali Kiba wameonyesha walikuwa na shauku kubwa ya kusikia
kazi mpya wa King Kiba.
Baadhi ya mashabiki wa Kiba
wameitabiria makubwa ngoma hiyo licha ya kwamba bado hawajaisikia na
kusema kuwa huenda unaweza kuwa wimbo wa Taifa tena kwa namna
utakavyotamba na kupokelewa mitaani.
Jumaa_salim "Hope
itakuwa nyimbo ya taifa kama zilizopita, mwenye kipaji ni kama
perfume lazima harufu isikike. Ali Kiba unajua"
Baby_anney "Jamani can't
wait maana napenda sana kazi zako hamna mfano wake my favorite
@officialalikiba"
Frank Mugasa "Yani
naisibiri kwa hamu ngoma iyo inipoze machungu ya kufungwa na monaco"
Moja ya mstari ambao
unapatikana katika kazi mpya ya Alikiba unasema "Kama mapenzi
ghorofa yamejaa Kariakoo"
Ali kiba aliachia nyimbo zake
mbili Kimasomaso na Mwana tarehe 25/July/2014 baada ya kimya cha muda
mrefu na baadae kuna nyimbo mbili zilitoka ambazo kwa mujibu wa Ali
Kiba alidai kuwa hakuzitoa bali zimevuja ila alidai kuwa
atakachokifanya ni kuzifanya nyimbo hizo ziwe katika kiwango kizuri
ili ziweze wafikia mashabiki kwa ubora zaidi na ziweze kuchezwa
katika vituo mbalimbali vya redio..
0 comments:
Post a Comment