Kipigo
cha goli 1-0 kutoka kwa Mgambo JKT kimeonekana kumchanganya kocha wa
klabu ya Simba, Zdravko Logarusic, ambaye amekiri kuwa kikosi chake
kina kazi kubwa mbele ya Mbeya City katika mechi ijayo ya Ligi Kuu
Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Jumamosi hii.
Simba
juzi ilikutana na kipigo cha 'kustusha' kutoka kwa timu iliyokuwa
inaburuza mkia ya Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa na
hivyo kuteremka kwa nafasi moja kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi
ya tatu hadi ya nne ikiwa na pointi 31, tatu nyuma ya Mbeya City
iliyo katika nafasi ya tatu.
Loga
alisema kuwa baada ya kipigo hicho, timu yake ipo kwenye wakati mgumu
kwa sasa wanapoenda kucheza dhidi ya Mbeya City ugenini katika uwanja
"mgumu kupata matokeo" wa Sokoine.
Loga
alisema kama wangepata ushindi kwenye mechi yao ya juzi ingekuwa
chachu ya ushindi kwenye mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya City.
0 comments:
Post a Comment