Sakata
la wabunge kutaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Tamisemi), limechukua sura mpya, baada ya Waziri Mkuu
Mizengo
Pinda kuwataka wabunge wamtoe madarakani kama wanaona hafai.
Kauli
hiyo imetolewa leo bungeni wakati waziri mkuu alipokuwa katika
Kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu ndipo alipotoa kauli
hiyo na kuongeza kuwa kama itakuwa hivyo yeye atafurahi kwani atakuwa
amepata nafasi nzuri ya kupumzika na kuendelea na maisha yake ya kila
siku.
Halii
hii imefikia kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wabunge walikomalia
suala la kutaka Waziri mkuu na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu
wajiudhulu nyazifa zao kutokana na kushindwa kuchukua maamuzi dhidi
ya ubadhilifu wa Fedha katika Wizara yao.
Jumamosi
iliyopita, wabunge wawili, mmoja wa CCM, Kangi Lugola, (Mwibara) na
David Kafulila, (NCCR-Mageuzi Kigoma Kusini), walimlipua bungeni
Waziri Mkuu Pinda, wakimweleza kuwa ni mzigo namba moja na wamemtaka
Rais Jakaya Kikwete amtimue kazi.
0 comments:
Post a Comment