Tuesday, December 10, 2013

MCHAKATO SHINDANO LA MAISHA PLUS UMEIVAA

Lile Shindano ambalo linakutanisha Vijana na kuishi katika Kijiji cha Maisha Plus huku wakionesha ujuzi wao katika kukabiliana na Maisha ya kila siku kufuatia changamoto wanazokumbana nazo wakiwa hapo kijijini,huku wakipata nafasi ya kuonesha Vipaji vyao mbalimbali katika Kijiji hicho.

Maisha Plus ambayo inaendeshwa na Masoud Kipanya inatoa nafasi kwa Vijana ambao wanahitaji kujiunga na kwenda kuonesha uwezo wao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoonyesha uhalisia wa Maisha kwa namna moja au nyingine na kutoa nafasi kwao kuonesha uwezo wao kulingana na Vipaji vyao.

Kwa mujibu Masoud Kipanya amesema kuwa kwa sasa fomu ya kujiunga katika kijiji cha Maisha Plus zimeanza kupatikana sehemu mbalimbali.


0 comments:

Post a Comment