Monday, November 4, 2013

YANGA KUHARIBU MIPANGO YA MBEYA CITY

Ikiwa imebaki siku moja kwa Timu zinazoongoza Ligi Kuu Vodacom Bara Azam FC na Mbeya City kukutana na kuoneshana uwezo kisoka katika uwanja wa Azam
Complex(Chamazi) Mbeya City imetaka mechi hiyo kusogezwa mbele ili kupisha Mechi ya Yanga na JKT Oljoro itakayochezwa Siku hiyohiyo ya Alhamisi Uwanja wa Taifa.

Uongozi wa Klabu ya Mbeya City umesema unataka mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC iliyopangwa kufanyika Alhamisi wiki hii katika Uwanja wa Azam Complex (Chamazi), isogezwe mbele huku ukifanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Henry Kimbe, alisema watawasilisha barua yao kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuomba kufanyika kwa mabadiliko hayo hasa kutokana mazingira halisi yanayozunguka mchezo huo.

Kimbe alisema wanaamini mchezo huo utavuta mashabiki wengi wa soka wa jijini Dar es Salaam na kwamba kama utachezwa Alhamisi, utawafanya mashabiki wengine kwenda Uwanja wa Taifa kuiangalia Yanga itakayokuwa inacheza na JKT Oljoro siku hiyo.

"Kwetu tumefikiria na kuona kuna ulazima wa mabadiliko, tunataka kuwapa burudani mashabiki wetu, ikichezwa Chamazi itakuwa tatizo. Tunataka watu wa mjini watuone," alisema katibu huyo.

0 comments:

Post a Comment