Mkali
wa Bongo Movie ambaye kwa sasa anatamba na movie yake ya Foolish Age
Lulu Michael amefunguka na kusema kuwa watu wa magazeti wanamuandika
kila siku mara leo Kachumbiwa,mara kaolewa mara kaachika wanafanya
kumuandika vile watakavyo wao kwa malengo yao.
Lulu
amefunguka hayo baada ya Mtangazaji wa kituo kimoja cha Radio
kumwambia kuwa ameona Gazeti moja la LEO likiwa na habari ya Juu
kabisaa kuwa Lulu Michael amechumbiwa.
“nimesoma
kwenye gazeti la Leo tena front page "Lulu Achumbiwa"
nikajishangaa eti nikapata na wivu” alifunguka B12.
Kufuatia
Habari hiyo aliyoipata kupitia kwa Mtangazji huyo Lulu aliongeza na
kusema kuwa mbona hao waoaji hawafiki kwa Mama yake na kujitambulisha
rasmi ikifahamika au wanaoa wakiwa ndotoni?aliuliza.
“mbna
hao wachumbiaji hawafiki kwa mama lulu!?wananichumbia ndotoni ama!?”
Mwishoo
wa siku alimaliza kwa kusema haya hao magazeti
wananichumbia,wananioa,wananiacha yani t depends na mood walio amka
nayo!wanaamua tu







0 comments:
Post a Comment