Thursday, November 21, 2013

SIMBA WATENGUA KAULI YAO RAGE AREJESHWA TENA

Bodi ya wadhamini ya klabu hiyo imetangaza kusitisha maamuzi ya kamati yao ya utendaji ya kumwengua katika nafasi uenyekiti.
Jumanne Kamati ya Utendaji ya Simba iliyokutana Jumatatu bila uwapo kwa mwenyekiti (Rage) aliyekuwa Marekani, ilitangaza kumsimamisha Rage na makocha wa timu yao, Abdallah 'King' Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelu 'Julio'.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, Hamisi Kilomoni, alisema katika kikao hicho cha bodi kilichohudhuriwa na wajumbe wawili (Kilomoni na Ramesh Patel), kilisitisha maamuzi ya kumsimamisha Rage kwa sababu kikao kilichokaa na kutoa maamuzi hayo kilikuwa ni batili.

Kilomoni alisema pia kuwa, wameamua kusitisha maamuzi hayo ili kuiepusha klabu hiyo na migogoro ambayo inaweza kuanza kutokana na hatua hiyo ya kumsimamisha mwenyekiti wao.

0 comments:

Post a Comment