Msanii
Prof Jay alimarufu kama Heavy Weight Mc ambaye anakubalika na kufanya
vizuri katika Kazi yake ya Sanaa hususani awapo stejini,amefunguka na
kusema kuwa Mashabiki wake ndio wanamfanya aendelee kuwa Vizuri
katika Game na hata katika Maisha ya kawaida.
“Asanteni
sana MASHABIKI wangu kwa kunisupport na kunifanya kuendelea Kuwa hivi
mpaka Leo... Naamini siwezi Kuwa Mimi bila nyinyi... I love u all na
nawaahidi sitawaangusha!!!! BLESS.”
Prof
Jay kwa sasa hana nyimbo mpya ambayo lakini ni moja kati ya wasanii
waliopiga Show Nyingi ambazo kwa Mwaka huu na kuweza kumfungulia
Milango mingi ya Mafanikio,japo kuwa mkali huyu hana nyimbo mpya
Radioni lakini asimamapo Jukwaani huwapagawisha Mashabiki wake kwa
kazi zake zilizofanya Vizuri miaka ya Nyuma na kujikuta akiteka Hisia
zas Mashabiki wake hao na kwenda nao pamoja katika Kila mstari na
kila Wimbo atakaoimba kwa Steji.
Prof
Jay ni moja kati ya Wanamuziki wa Zamani ambaye ameweza kuwa na
mafanikio kutokana na kazi yake ya Sanaa mbali na kumiliki Usafiri
lakini amefanikiwa kujenga nyumba ya Kisasa Mbezi,na kumiliki
Biashara mbalimbali ikiwemo Saloon ambayo ipo Maeneo ya Msasani na
kufungua Studio kwa ajiri ya Kurekodi Muziki ambayo mpaka sasa
haijaanza kazi Rasmi.
0 comments:
Post a Comment