Mshambuliaji
Hamis Kiiza wa Yanga yupo katika wakati mgumu wa kusugua Benchi ndani
ya Kikosi cha Yanga baada ya Kumzingua Kocha Mkuu wa Yanga
Mholanzi
Ernie Brandts kwa kumzushia maneno na kumporomoshea Maneno yenye
shombo kocha huyo baada ya Kumalizika kwa Mzunguko wa kwanza wa Ligi.
Kwa
mujibu wa Vyombo vya Habari viliwanukuu Didier Kuvumbangwa na Hamis
Kiiza kuwa Kocha wao anakinyongo nao hivyo anawapa Muda mdogo wa
kuonesha uwezo wao wawapo uwanjani,kutokana na hali hiyo imemlazimu
Kocha huyo kutoa tamko kuwa hayupo teyari kumpa Namba Mchezaji
asiyefuata maagizo na asiyejituma katika Mazoezi.
Sitaangalia jina la mchezaji, Yanga ina wachezaji wengi, tutatumia walio tayari kufuata maelekezo ya benchi la ufundi," Brandts.
Mbona Kuvumbagu Humzungumzi na wote wamefanya makosa sawa?
Kuhusu swali hili Kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Brandits alifunguka na kusema kuwa
"Nimezungumza na Kavumbagu (Didier), ameniomba msamaha kutokana na alichokifanya na nimemkubalia kuendelea na mazoezi ya timu. Kiiza (Hamis) bado sijamwona na sijazungumza naye chochote kwa sasa,"
0 comments:
Post a Comment