Thursday, November 28, 2013

FAHAMU MUDA AMBAO KOMBE LA DUNIA LITAKUWEPO UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI HII.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Coca-Cola ambayo ndiyo imefanikisha kwa Kombe la Dunia Kufika Tanzania na kuwapa nafasi Watanzania kuweza kupiga nalo picha
na kulishuhudia Live siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa.

Kombe hilo la Dunia litaingia Uwanjani Muda wa saa 3:00 Asubuhi Mpka saa 12:00 Jioni na kutoa fursa kwa Raia wanaopenda Michezo kushuhudia Kombe hilo na kupata nafasi japo ya Kupiga nalo Picha kama Ukumbusho .

Hakutakuwa na Kiingilio chochote kwenda kulishuhudia Kombe hilo na kutakuwa na Burudani mbalimbali ambazo zimeandaliwa kwa wale watakaoweza kufika Uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi.


0 comments:

Post a Comment