Mwanafunzi
aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Sabasaba mjini
Iringa akijiandaa kurudia kufanya mtihani wa taifa
wa kidato cha nne kupitia kituo
cha Krelluu mjini
Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika
manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa
kile alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara
mtihani wa kidato cha nne.
Katika
barua yake ndefu aliyoiandika kijana huyo
amesema kuwa amefanya hivyo si kwa kujipendea ila
amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara hivyo
kuamua kujiua ili kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao
anaamini angefeli.









0 comments:
Post a Comment