Wednesday, November 6, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMATANO: 6/11/2013

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Siku ya leo unawaza juu ya safari, au kupata mwanamke au mwanamme, bwana au bibi aliyembali na mliopotezana aje au upate habari zake, unapenda taabu ya
mwanamke au ugonjwa alionao uondoke, unawaza vile vile juu ya ndugu zako namna ya kuwasaidia ili waongoke. Kila jambo isipokuwa la ndugu zako litafunguka.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo una Mawazo juu ya fitina uliyofanyiwa na tofauti juu ya pesa au kitu au kazi. Unayo fikiri kuhusu taabu zako, mwanamke au mwanamme wako ametoroka na kuna au ugonjwa. Una wasiwasi juu ya Kesi huenda ikakushika kuhusiana na pesa kazini kwako.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo utapata habari juu ya wazee ambao ni wagonjwa au wamepatwa na jambo la kutisha. Inaonekana una mawazo juu ya kupata bahati ya safari, au unaingoja kwa hamu kubwa safari hiyo ambayo itakuwa na faida kwako.Unataka sana mtu umpendae au kitu ukipendacho kije na unategemea barua nzuri au ujumbe.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Hivi sasa au Leo utakabiliana na adui yako mkubwa sana au utapata habari ya ugonjwa au wewe mwenyewe kuugua .Unakabiliwa na taabu kubwa ya mkeo au mumeo hasa juu ya mambo ya pesa au kazi au biashara

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo Mawazo yako ni juu ya pesa, kazi au kitu. Unafikiria kukutana na rafiki zako ambao wana mali au biashara na unatarajia kupata mali, biashara au kazi kutoka kwao.
Yote unayoyataka yatapatikana kati ya leo na Jumapili asubuhi Jaribu kufuatilia

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Siku ya leo zipo habari za kukufurahisha ambazo unazingojea. Hivi sasa inaonekana una mgogoro na mpenzi wako au rafiki yako au zipo tofauti kubwa kati yako na mkeo au mumeo au mtu mnaeshirikiana nae katika kazi au Biashara. Jaribu kumaliza tofauti hizo au utakwama.

NG’OMBE – TAURUS (APR 23 – MAY 20)
Unafikiria sana juu ya safari au kupata barua. Inaonekana kuna ushindani au uadui mkubwa juu ya mali au kitu. Una mawazo juu ya mgonjwa unayemuuguza. Vile vile unamfikiria mtoto wako aliye mbali na furaha au ndoa. Unataka sana kupata pesa au kazi. Kutana na wakubwa wakusaidie

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo una mawazo ya kuhama hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine kwani hiyo ndio tabia yako. Wiki hii utapata habari ya wizi na kufiwa au utapata wageni au utasikia maneno mengi yatakayokuudhi, Mambo hayo yatakutokea kat ya leo na Jumatatu

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Inaonekana leo unafikiria sana juu ya ndugu zako, mpenzi wako au Mumeo au Mkeo. unataka kufanya sherehe kubwa sana kwa ajili yao. Hivi sasa unasumbuliwa na kesi inayohusiana na ndoa au juu ya watu unaoshirikiana nao katika kazi au biashara. Mambo yote ni mabaya wiki hii.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Tatizo lako hivi sasa ni juu ya maneno maneno yaliyotokea kuhusu pesa. Inawezekana ukasimamishwa mbele ya hakimu au mpatanishi. Kazi kwako pia tahadhari kuna maneno na watu wengi wanaitaka kazi hiyo. Ndugu yako mwanamke hivi sasa yupo katika taabu nenda kamsaidie. Kuwa muangalifu huenda pia mumeo au mkeo akakuletea taabu.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Wiki yote hii una mawazo juu ya mtoto, au mpenzi au habari ya pesa ama kazi. Huenda kuna kitu fulani kikapotea au pesa kuibiwa au kazi kukutoka. Nakuona pia una maneno au kesi na mwanamke au mwanamme huenda kesi hiyo ni ndoa au Talaka. Kuwa muangalifu inaonekana kuna mikwamo itakujia.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo utapata au umepata habari ya mgonjwa. Vile vile kuna habari ya wizi wa pesa, udanganyifu na kuharibika kwa biashara au kazi. Unafikiria sana kukutana na rafiki yako mpenzi, Safari yako endelea nayo na utapata faida kubwa.


Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Husein

0 comments:

Post a Comment