NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo utafanikiwa baada ya kusumbuka kwa muda mrefu tumia
utakachopta kutumia na wengine usiwe mbahil, lakini elewakwamba mambo
yako yamo hatarini kuharibiwa na watu, unatakiwa kuwa mpole kwa muda
huu ili kupisha dhahama hiyo.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES
23)
Siku ya leo usipokuwa makini kipato chako kitapotea bila
kujua na wiki hii unashauriwa kutosafiri ili kujikinga na mabalaa
katika safari hizo. Jaribu kuwa muangalifu na yoyote
utakayeshirikiana naye ili kuokoa kile ambacho kitasalia
MBUZI
- CAPRICORN (DES 22 – JAN 20
Leo hii tafuta njia zaidi za
kukusaidia, marafiki na majirani wa karibu wanaweza kutoa mchango
mzuri , kuna dalili ya kufanikiwa katika mambo yako, unashauriwa
kuutumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umeyapanga
kuyafanya.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Leo ni
siku mbaya kwako inaonekana shughuli zako zinaweza zikakumbwa na
dosari kuna uwezekano wa kupata mkosi kazini kwako au utaletewa
biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha. Jaribu kuwa muangalifu
mipango yako yote uliyoipanga hasa leo achana nayo.
SAMAKI –
PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo hii katika biashara zako utapata
faida ambayo hukuitegemea na yule rafiki yako uliyemkosea utakusamehe
madhambi uliyomfanyia. Jitahidi kukutana na wakubwa zako wakusaidie
kupata ushauri.
PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Pamoja na
kwamba leo inaweza kuwa siku njema kwako utapatwa na mambo ya ajabu
ajabu, mambo hayo yatakushangaza usijaribu kujibishana na watu
usiowajua kunaweza kutokea ugomvi mkubwa.tegemea kupata safari ya
itakayokupeleka sehemu ambayo hujawahi kufika.
NG’OMBE –
TAURUS (APR23 – MAY 20)
Usiendekeze mambo makubwa kwani unaweza
kujikuta ukiingia kwenye matatizo na kupata hasara, upo uwezekano wa
kukutwa na balaa huko uendako.kuna uwezekano wa kutokea matatizo
kazini kwako au kwa mtu anayekuhusu,
MAPACHA - GEMINI (MAY
23- JUN 23)
Vikwazo havitakosa kukuandama siku ya leo unaweza
kujikuta hata wale uliowategemea sana katika utekelezaji wa mambo
yako nao wakakuweka kwenye wakati mgumu
KAA – CANCER (JUN
22 – JUL 23) yoendelea kukupotezea
Jumanne ya leo usisumbuke na
mambo madogo madogo ambayo yanayoendelea kukupotezea mudaa ni wakati
wa kuangalia mbele, uhusiano wako na mtu uliyempata hivi karibuni awe
ni mpenzi au rafiki utavurugika, Unashauriwa kuwa makini na hao
marafiki wapya watakaokujia siku za karibuni.
SIMBA – LEO
(JUL 24 – AUG 23)
Jumanne ya leo jitihada zako ndizo
zitakazokufanya wewe kufanikiwa kirahisi, jaribu kuwa karibu na watu
wa dini ili kubrilikiwa mambo yako.Kazi nyingi nzito na ahadi kibao
zisizitekelezeka zinaweza kuwa kikwazo.
MASHUKE – VIRGO (AUG
24- SEPT 23)
Leo hii ni siku muhimu sana kwako kuwa muangalifu,
faida utakayopata katika mambo yako isikufanye ukabweteka na kufanya
dharau kwa watu wengine,ikitokea siku ya leo ukikutana na mtu ambaye
hana miguu kabisa, hiyo ni dalili kuibiwa mali yako au kupoteza vitu
vya thamani kubwa,
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Leo
fanya uchunguzi wa mambo unayoyatilia mashaka, jaribu kuwa karibu na
wale ambao unahisi wanaweza kukupa msaada jihadhari na vikundi
visivyofaa hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili
wakusaidie.
0 comments:
Post a Comment