NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu na mpenzi wako au rafiki yako kwani wanampango wa kukugeuka na kukudhulumu, fanya mambo yako bila ya
kuwashirikisha kwa kipindi hiki. Wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu na mpenzi wako au rafiki yako kwani wanampango wa kukugeuka na kukudhulumu, fanya mambo yako bila ya
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo utakuwa katika wakati mgumu mno wa kuamua jambo ambalo umeshawishiwa na mpenzi wako au rafiki yako wa karibu, kuwa mwangalifu na uamuzi utakaouchukua. Lazima katika mambo yako uwashirikishe wazee ndio utafanikiwa.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo Jaribu kuwa mwangalifu sana, watoto wako wana mpango wa kukudanganya na kuna uwezekano wa kufanya mambo kwa kushirikiana na adui zako baada ya kushawishiwa kukufanyia ubaya.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Ikitokea leo wakati wowote ukaona kitu cha kukushangaza, au kitu ambacho unahisi hujakiona maishani mwako, hiyo ni dalili ya kupona maradhi yako ambayo yamekuwa yakikusumbua kwa muda mrefu.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo akikujia mtu akataka Mazungumzo ya aina yoyote kutoka kwako, hiyo ni ishara ya kwamba leo utatukuzwa kwa jambo utakalolifanya na utapata matatizo katika malengo yako uliyoyapanga kwa wiki nzima.
PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Leo ukikutana na mtu akakusimamisha, hiyo ni dalili ya kujipatia upendeleo fulani katika shughuli zako za kila siku pia kama mtu huyo ni mwanammke basi hiyo ni dalili ya kupata cheo.
NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Kama Leo akikujia Mkweo au ukipata salamu za mwanao , hiyo ni dalili ya kupata Safari ndefu, utapata kitu kizuri au biashara zako zitakuendea vizuri, Unashauriwa kuwa mkarimu kwa kila atakaekujia na shida yake.
MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo unatakiwa kufanya mambo mapya ili kujipatia kipato, mambo yako ya zamani ni bora ukayaacha kwanza au kuyapanga upya. Unashauriwa kuwatembelea wazee wako ili kupata baraka zao kwa kila jambo unalotaka kulifanya.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo mambo yako yatakuendea kama ulivyopanga bila ya kuingiliwa na mtu au vikwazo vyovyote, uhusiano ambao umevurugika kati yako na Mpenzi wako sasa utatengemaa.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo ukikutana na mtu mwenye nywele nyingi, basi hiyo ni dalili ya kupata kila kitu ulichokuwa unakitaka kutoka kwa mpenzi wake, vile vile ni dalili kuwa mpenzi wake sasa ametulia na mambo yao yatawanyookea.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo Ukimuona Mwanamke ananyonyesha hiyo ni dalili kuwa mambo yako ya kimapenzi sasa yatageuka na kuwa ya kugombana gombana, unashauriwa kuwa mtulivu na kutotaka kujibishana kila wakati.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Siku ya leo unatakiwa kuwa mwangalifu sana kwa kila jambo analotaka kulifanya hasa linalohusiana na pesa vinginevyo ipo hatari ya kupatwa na balaa. Pata ushauri wa kisheria kwa kila jambo unalotaka kulifanya.







0 comments:
Post a Comment