Wakali wa kucheza bila
kukunja Goti Mwanafalsafa na AY ambao Mwanzo walikuwa na tofauti
kidogo na Produza Hermy B aliyetengeneza ngoma zao kama
Habari ndiyo
hiyo,Nangoja ageuke na zingine ambazo zilitengenezwa ndani ya B Hits
,wameweka tofauti zao kando na kuishi tena kama Rafiki kama Zamani.
Kupitia Ukurasa wa
Facebook wa Produza Hermy B alionesha kuwa sasa wameamua kumaliza
Tofauti zao na kurudia maisha yao ya awali ambapo waliishi kama
Marafiki waliokuwa na upendo baada ya kuandika Ujumbe Mfupi
uliosomeka
‘Friends again’,
huku akiwa ameambatanisha na Link
ambayo inaonesha Picha ya Pamoja ya Hermy B,FA na AY
Picha hiyo inaonesha
Hermy B amemwagiwa Maji inasemekana alimwagiwa ndoo ya maji katika
kusherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini kuthibitisha hilo Hermy
alipost Picha Nyingine ikimuonesha yupo na FA Uwanja wa ndege JNI na
kuandika maneno machache yalisomeka hiviiii‘Bday continues’.
Mpitanjia inatoa
pongezi kwa rafiki hawa ambao waliweza kushirikiana vizuri mwanzo
kikazi zaidi na kufanikiwa kundondosha Ngoma nyingi zilizotingisha
africa Mashariki kwa kumaliza tofauti zao.
0 comments:
Post a Comment