Sunday, December 1, 2013

HUYU NDIYE MMOJA KATI YA MWANAMKE WAWILI WALIOKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Jeshi la Polisi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), linawashikilia wanawake wawili ambao ni wafanyabiashara wa kigeni kwa tuhuma za kukutwa
wakisafirisha kilo 12.7 za dawa za kulevya maarufu kama 'unga'.

Watuhumiwa hao waliokamatwa jana alfajiri katika uwanja huo ni Josiane Dede Creppy (25), raia wa Togo na Grace Teta (34), raia wa Liberia ambao kwa nyakati tofauti, mmoja akijiandaa kuelekea jijini Accra, Ghana na mwingine nchini Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, aliiambia NIPASHE jana kwamba mtuhumiwa Grace alikamatwa akiwa na kilo 10.5 za dawa hizo wakati  akisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision Air kutoka KIA kwenda Captown nchini Afrika Kusini kupitia Nairobi, Kenya.


“Huyu alikamatwa na unga unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya alfajiri ya saa 10:45 akitumia hati ya kusafiria yenye namba 1039080 ikimuonyesha ni mfanyabiashara na raia wa Liberia. Josiane alikamatwa saa 8:50 alfajiri akiwa na kilo 2.2 za dawa hiyo akiwa anataka kuondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia kelekea Ghana,” alisema Kamanda Boaz.


Chanzo:Nipashe.

0 comments:

Post a Comment