Kocha
mpya wa Simba, Zdravok Logarusic, raia wa Croatia amewasili nchini na
anatarajia kusaini mkataba wa kukinoa Kikosi
cha Wanamsimbazi hao
leo ambao utakuwa na thamani ya shilingi milioni 57.6.Kocha huyo aliyewahi kuinoa Gor Mahia ya Kenya anakocheza kipa Mtanzania Ivo Mapunda, aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana asubuhi na alitumia siku nzima ya jana kupitia mkataba wake mpya na Simba kabla ya kuutia saini leo.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema uongozi wa klabu hiyo utakaofuatana na kocha huyo, utazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu ujio wa kocha huyo.
"Kila kitu kitaelezwa LeoTutawaeleza tumeingia naye mkataba kwa kipindi kipi," alisema Mtawala, Wakati Mtawala akiyasema hayo, chanzo cha ndani ya klabu hiyo kocha huyo atasaini mkataba wa mwaka mmoja na atakuwa akilipwa Dola 3000 za Kimarekani kwa mwezi ambazo ni sawa na shilingi milioni 4.8 za Tanzania, hivyo ndani ya mwaka mmoja atakuwa anapokea shilingi milioni 57.6.
0 comments:
Post a Comment