Mchezaji Kiraka
Yanga
Mnyarwanda Mbuyu Twite amechomolewa katika Kikosi cha Timu ya Taifa
ya Rwanda kutokana na kukaidi Agizo lililomtaka kurudi
Rwanda katika
Timu ya Taifa kuisaidia timu yake ya Taifa dhidi ya Mali.
Kocha Mkuu wa Timu ya
Taifa ya Rwanda Eric Nshimiyimana, amesema hana mpango na mchezaji
huyo baada ya kumwita kwenye mechi dhidi ya Mali akakaidi na kuzima
simu.
“Ni tabia mbaya kwa
mchezaji kuitwa na kukaidi, kocha hawezi kumnyenyekea mchezaji mmoja
kwenye timu ya Taifa. Nafasi ya Mbuyu imeshazibwa na vijana wadogo
ambao wanafanya kazi kikamilifu.
“Hatuwezi kuendelea
kuendekeza hizo tabia, tuna wachezaji kama wanne wadogo ambao
wanaweza kufanya kazi vizuri kabisa, hakuna haja ya kuangaika na
Mbuyu.”
Kutokana na mazingira
hayo kwa sasa Beki huyo anayekipiga katika Klabu ya Yanga hawezi
kupata nafasi kirahisi kurudi katika Kikosi cha Taifa katika Timu ya
Rwanda.
Source:Mwanaspoti.
0 comments:
Post a Comment